Zanzibar Police College

Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kuipongeza timu nzima iliondaa website hili chini ya ofisi ya habari na mahusiano ya chuo (DPA).

Ni ukweli usiopingika kuwa katika ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia, suala la ushirikiano na ubia kati ya taasisi moja na nyingine ni suala mtambuka, na usiokwepeka. Mojawapo ya njia ya kudumisha mahusiano na jamii na wadau mbalimbali ni kujenga mahusiano bora, website hii linalenga kuitambulisha jamii ya DPA kwa wadau mbalimbali na kwa jamii nzima kwa ujumla.

Kupitia maandiko na picha mbalimbali katika website hii  naamini vitakuwa sehemu ya mafunzo, na ushirikishwaji wa taarifa  kwa wadau mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi na nje ya Jeshi la Polisi.

Hivyo naamini kila atakaetembelea webiste hii basi atajisikia kuwa ni sehemu katika jamii ya wanataaluma wa Jeshi la polisi katika chuo cha Polisi Dar es salaam.