Zanzibar Police College

 

 

Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kuipongeza timu nzima iliondaa website hili chini ya ofisi ya habari na mahusiano ya chuo (DPA).

Ni ukweli usiopingika kuwa katika ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia, suala la ushirikiano na ubia kati ya taasisi moja na nyingine ni suala mtambuka, na usiokwepeka. Mojawapo ya njia ya kudumisha mahusiano na jamii na wadau mbalimbali ni kujenga mahusiano bora, website hii linalenga kuitambulisha jamii ya DPA kwa wadau mbalimbali na kwa jamii nzima kwa ujumla.

Kupitia maandiko na picha mbalimbali katika website hii  naamini vitakuwa sehemu ya mafunzo, na ushirikishwaji wa taarifa  kwa wadau mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi na nje ya Jeshi la Polisi.

Hivyo naamini kila atakaetembelea webiste hii basi atajiskia kuwa ni sehemu katika jamii ya wanataaluma wa Jeshi la polisi katika chuo cha Polisi Dar es salaam.

Chuo cha taaluma ya Polisi  Dar es salaam kimejikita katika kutoa elimu katika nyanja mbalimbali za kiulinzi na kiusalama, lakini pia kufanya tafiti mbalimbali katika masuala yanayohusiana na ulinzi na usalama ili kuweza kuwa na taifa lenye hali ya amani na utulivu. Hivyo niwahikikishie wadau wetu wote kuwa chuo kimejipanga vyema kuweza kuwa chuo cha mfano katika kuwajengea uwelewa maafisa wa polisi na raia katika kudumisha haki, amani na usalama  katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

 

Karibuni DPA, kitivo cha maarifa ndani ya Jeshi la Polisi !

LAZARO B. MAMBOSASA (SACP)