Zanzibar Police College

OUTDOOR FACILITIES

Chuo cha DPA kina maeneo maalumu kwa ajili ya askari na maafisa wanaohudhuria kozi hapa chuoni. Baadhi  ya maeneo hayo ni uwanja wa parade   kwa ajili ya maonyesho mbalimbali pindi askari au maafisa wanapohitimu mafunzo yao. 

Pia chuo kuna meneo maalumu kwa ajili ya mafunzo ya porini (field craft training ground ) kwa askari na maafisa wa ngazi zote kwenda kujifunza kwa vitendo zaidi.

Mafunzo kwa vitendo ni  njia bora ya kumfanya askari kuwa mkakamavu zaidi, hivyo bhasi  wakufunzi huwa hodari zaidi na kuhakikisha askari anapokuwa mafunzoni  anawajibika na kutimiza wajibu wake.

Askari pindi anapomaliza mafunzo haya huwa hodari kwa ajili kutekeleza wajibu wake wa kulinda raia na mali zake.

Picha zinaonyesha Askari na maafisa wakiwa katika uwanja wa mafunzo kwa vitendo.

Parade

Field craft training ground